Latest Photos :
.

Tujipange Kutoa Warembo Kimataifa"Jackline Haider

MKURUNGEZI wa kampuni ya Allure International, Jaqualine Haider, inayojihusisha na masuala ya urembo, mitindo kwa muda mrefu, amesema kuwa mipango yao mikubwa ni kuinuka zaidi kimataifa ikiwa pamoja na kuwatoa wanamitindo wa Tanzania katika kutimiza malengo yao ya kifika kimataifa. Kampuni hiyo ni ya muda mrefu katika masuala ya urembo na ina matawi kadhaa nje ya nchi, ambapo mkurengezi wake anaamini kuwa kuwepo kwao katika tasnia hiyo kwa muda mrefu kumewawezesha kujua mambo mengi na kupata uzoefu katika kazi hiyo. Alidai kuwa hata hivyo kuna changamoto kubwa inawakabili kwa hapa nchini kwani warembo wengi wamekuwa wakipenda fani hiyo mitindo lakini ni wavivu kwa kujifunza zaidi. “Kila fani ina elimu yake hivyo ni vyema warembo wanaohitaji kuingia katika fani hii lazima wawe wepesi wa kujifunza mambo mbalimbali juu ya mitindo, pia lazima wakubali kusoma zaidi ili kuongeza ufanisi,” alisema. Hata hivyo Haider anaamini kuwa Tanzania ni moja ya nchi ambayo zinawarembo wengi ingawa baadhi ya wazazi wamekuwa vikwazo katika kuwatoa watoto wao kujiendeleza na fani hizi ambazo ziunaweza kuwa ajira.
Share this article :

Post a Comment

 
Support : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2011. Hot Girls Photos - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger Template